26/02/13

Testimonies of Transformation

Naitwa Julieth Mosha nina miaka 22

Nilikuwa mwanafunzi nilipofika kanisani kwa mara ya kwanza miaka
miwili iliyopita, nilikuwa nikitegemea wazazi wangu kwa kila kitu na
wakati mwingine hawakuwa na uwezo wa kunipatia kila kitu
nilichohitaji; ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu. Nakumbuka
kulikuwa na wakati nilikuwa nikitaka vitu muhimu sana kama vifaa vya
shule na hawakuweza kunipatia, hata ada ya shule ilikuwa ni
changamoto kwao, ulikuwa ni wakati mgumu kweli.

Ndipo dada yangu alinikaribisha kuja katika Kanisa la Universal la
Ufalme wa Mungu, ambapo nilijifunza kuhusu zaka. Ili kuwa ni vigumu
sana kwangu kuamini mara ya kwanza, hata nilifikiria kwamba
wachungaji walikuwa wanataka pesa yangu, niliposikia kwa mara ya kwanza kuhusu kumfanya Mungu kuwa wa kwanza, kuhusu kumrudia Mungu, kutenga asilimia 10 ya kwanza ya kila kitu ninachopokea na kuleta katika madhabahu ya Mungu, ilikuwa ni vigumu sana kuamini na kufanya hivyo, kwa sababu nilikuwa sina kitu hata kile kidogo nilichonacho bado natakiwa nitoe zaka! Lakini siku moja nilimsikia Mchungaji akisema tunapotoa zaka tunajaribu Mungu, kwa sababu ni mtoa zaka tu mwenye haki ya kumjaribu Mungu na Mungu hawezi kushindwa katika Jaribio.

Nikaamua kumjaribu Mungu na zaka yangu, nilitenga asilimia 10 ya kila kitu nilichopokea nani kaleta katika madhabahu ya Mungu, nikawa mtoa zaka mwaminifu tangia hapo mpaka sana Mungu ananiheshimu. Leo sitegmei wazazi wangu tena, nina kazi nzuri inayonilipa mshahara mzuri na nimefungua biashara yangu mwenyewe ambayo inakuwa siku hadi siku, maisha yangu yamebadilika kabisa, sasa hivi nina kila kitu ninacho taka na nina kipata muda ninaotaka na sasa hivi mimi ndiye ninaye wasaidie wazazi wangu na ndugu zangu.

Zaka kweli inafanya kazi!

Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu



Felista Raymond Tarimo

Nilikuwa mlevi zaidi ya miaka 10. Hali hii ilikuwa ikiharibu Familia yangu, watoto wangu and muonekano wangu.

Familia yangu ilikuwa ikinitegemea, kwa ajili ya Elimu, kuwapatia chakula na mavazi, lakini kila shilingi niliyoipata nilitumia kunywa pombe. Ili fika kipindi nilichoka aina ya maisha niliyokuwa nikuishi, kwa hiyo nikaenda kwa waganga kutafuta msaada; walinipa kila aina ya miti shamba ili niweze kuacha kunywa pombe lakini haikusaidia kitu.

Siku moja nilikaribishwa kuja katika Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu na nikaenda kanisani nikazungumza na Mchungaji nikamwambia kuhusu matatizo yangu, Mchungaji akaniambia kwamba maisha yangu yanaweza kubadilika. Akanishauri kuhusu mnyororo wa maombi wa Ijumaa saa 11:30jioni na Jumapili saa 4:00asubuhi.

Nilifuatilia mnyororo wa maombi kama ilivyoongozwa na nikapona mabadiliko maishani mwangu; Leo nipo huru kutoka kwenye ulevi wote, naweza kutunza familia yangu na matatizo niliyokuwa nayo mwanzoni sasa yameondoka yote. Hatimaye nipo huru!

Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu


Ennah Eliamini
Kabla sijaja katika Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu, nilikuwa na uvimbe kwenye koo nilienda kwa madaktari na hospitali nyingi Lakini sikupata suluhisho daktari aliniambia suluhisho pekee ni kufanyiwa upasuaji, nilimlilia Mungu nikamwambia kama uliweza kuwaponya wengi kwa nini usiniponye na mimi, ndipo siku moja nikasikia kuhusu Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu kwenye redio (kipindi cha Drying Tears kila siku saa 11 alfajiri 100.5 Times Fm) nikachukua uamuzi wa kuja nikashiriki kwenye maombi ya Jumapili saa 3:30 asubuhi sasa nimeponywa kabisa.

Kwa Kweli Mungu Yupo Hai!

Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu



Makao Makuu - Jengo la Rex Investment karibu na Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam na Tansoma Hotel makutano ya mtaa wa Makamba na Livingstone karibu na kiwanja cha Kidongo Chekundu -Gerezani (Kariakoo) – Dar es Salaam / 0715 523 469 – 0715 982 653

.

.